Monday, 1 April 2019

MUHTASARI WA KIKAO CHA KWANZA CHA WANACHAMA WOTE WA KIKUNDI CHA USHIKI.

  •  
                                                                           kilifanyika 03/07 /2018                 Siku ya JUMANNE                         Muda 11 :45 hadi12:45


      Tulikaa kikao cha kwanza cha wanachama wote maeneo ya MSALE HALL.
     Tukikuwa jumla ya wanachama 41ambao ni wanaume 8 na wanawake 33.

           
      AGENDA

  •      Kujadili kama wafanyakazi kuhusu kuanzishwa kikundi cha kimaendeleo chenye nia ya kushirikiana, kusaidiana katika mambo mbalimbali na kukuza kipato chetu. Kikundi ambacho kitaongozwa na kwa mujibu wa sheria na katiba. 
  •  Mtoa mada aliwataka wanachama wasimamie kamati ya muda itakayo simamia agenda za kikao.                                                                                                     Kamati ilipokea maoni (  AGENDA ) pamoja na maswali mbalimbali kutoka kwa wanachama.                                             i) KUUNDA KATIBA.                       ii) UENDESHWAJI WA KIKUNDI NA USIMAMIZI WA MALI.                                                          iii) HAKI ZA MWANACHAMA.                                     iv) JINA LA KIKUNDI.                     v) KUFUNGUA AKAUNTI. 


     KUUNDA KATIBA :
Kamati ilikusanya maoni ambayo ni.

Ukurasa wa kwanza, Utangulizi, jina la kikundi, Malengo ya kuanzisha kikundi, Aina ya wanachama, Haki za wanachama na ukomo wao, Muundo wa viongozi sifa na wajibu wao, mikutano ya kikundi na kazi zake, usimamizi wa fedha, Vyanzo vya mapato ya kikundi, Mwaka wa fedha wa kikundi, Ukomo wa kikundi, Majina ya wanachama waanzilishi na vyeo vyao na anuani zao.

  UENDWESHWAJI WA KIKUNDI NA USIMAMIZI WA MALI.
 Wanachama waliamua kwa pamoja kuwe na kiwango maalumu ambacho kitalipwa kila baada ya wiki mbili (02) ambacho ni 10000/= Tsh

 Wanachama walikubaliana kwa pamoja Kiwango cha fedha kiwe kimoja kwa kila mwanachama.

 Wanachama walikubaliana kwa pamoja kuunda kamati ambayo itasimamia mchakato mzima wa katiba.

  Usimamizi wa mali za kikundi utakuwa chini ya kamati ambayo wakishirikiana na viongozi.


 HAKI ZA MWANACHAMA
 - kugombea nafasi yeyote ya uongozi na kuchagua au kuchaguliwa.
 - Kila mwanachama anakula moja ya siri na mwenyekiti ana kula moja ya turufu katika kutatua  maamuzi yanayo fungamana.
 - Kabla mwanachama hajafukuzwa anayohaki ya kupeleka utetezi wake mbele ya mkutano mkuu ambao utazingatia utetezi huo kabla ya kutoa maamuzi.
 - Mwanachama akijitoa mwenyewe kwa hiari yake atapigiwa hesabu na kulipwa stahiki zake kulingana na makubaliano ambayo yatafanywa na mkutano mkuu.
 - Kupata huduma zote zinazopatikana ndani ya kikundi.
 - Kupeleka malalamiko katika kamati ya nidhamu.
  - Kuhudhuria kwenye matukio mbalimbali (Misiba, Sherehe, Miradi).
 - Kupewa taarifa ya mapato na matumizi.
 - Kutoa maoni kwa uhuru na kusikilizwa.


 JINA LA KIKUNDI.
 Wajumbe walipendekeza majina matano (05) ambayo ni.

°Garden.
°Nia njema.
°Ushiki.
°Fikra mpya.
°Funga mkanda.

 Ambayo yalipigiwa kula yakabaki matatu (03)

°Nia njema.
°Fikra mpya.
°Ushiki.

Jina lililopatikana ni ;
   USHIKI


 KUFUNGUA AKAUNTI.
 Wanachama walikubaliana kufungua akaunti ya kikundi ambayo itatumika kutunza mapato yote yatakayo patikana kutoka kwa wanachama, Miradi pamoja na wadhamini.

Waliamua fedha zote zitunze katika benki ya NMB.

Walichagua majina ya wajumbe watakao tia saini benki  ambao ni.


  1. JUDITH OSTAY MBYALU 
  2. NASRA AMIRI RAJABU 
  3.  ASMA GOMBERA 

 KUFUNGA KIKAO ;
 Mwenyekiti wa kamati ya muda aliwashukuru wanachama kwa niaba ya kamati yake kwa kufanya uteuzi wa kamati na kutoa mawazo katika kikao hicho na kutangaza tarehe ya kikao kijacho ambayo ni  21/07/2018  na kutaja agenda za kikao kijacho na kufunga kikao. 

5 comments:

KARIBUNI KATIKA BLOG HII YA USHIKI GROUP.

USHIKI GROUP    ni blog ya kikundi cha USHIKI   kilichopo wilaya ya ILALA  kata ya TABATA mtaa wa MATUMBI makao makuu yake yapo MATUMBI.  ...